nhif new 71Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umezindua Baraza la Wafanyakazi ambalo ni chombo muhimu cha kushirikisha watumishi katika maamuzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umezindua Baraza la Wafanyakazi ambalo ni chombo muhimu cha kushirikisha watumishi katika maamuzi yautekelezaji wa malengo ya Mfuko huo.

Baraza hilo lililozinduliwa Mei, 23, 2015 litakuwa ndiyo chombo kikuu cha majadiliano ya kiutendaji baina ya uongozi wa Mfuko na watumishi kupitia uwakilishi wa wafanyakazi wa kila Kurugenzi, Idara na Ofisi za mikoa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo, Waziri  wa Kazi  na Ajira, Gaudensia Kabaka alisema kuundwa kwa Baraza hili ni hatua muhimu kwa Mfuko katika kutekeleza maagizo ya Serikali ambayo imekuwa ikisistiza juu ya umuhimu wa uwepo wa mabaraza hayo katika sehemu za kazi.

Aliongeza kuwa anaamini kuundwa kwa chombo hicho kutaharakisha utekelezaji wa malengo ya Mfuko kwa kuwa yatakuwa yanajadiliwa kwa pamoja baina ya uongozi na wafanyakazi ambao ndio watekelezaji wa kazi za kila siku.

Kabaka aliongeza kuwa wafanyakazi walitumie Baraza hilo kama chombo rasmi cha kuwasilisha mawazo  yao kwa uongozi  ili  yafanyiwe kazi kwa manufaa ya wanachama ambao wamejenga imani kuwa kwa Mfuko huo.