Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ni mfumo habari ya kikompyuta ambayo hutumika kurahisisha mawasiliano, utendaji wa kazi, utunzaji wa kumbukumbu na utoaji wa taarifa, lakini pia uwezo wa utambuzi.

Kupitia TEHAMA upashaji wa habari unakuwa rahisi na wa uhakika hivyo kurahisisha utendaji wa kazi za kila siku. Kwa kuliona hilo, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umeamua kwa dhati kujikita katika matumizi yake katika shughuli za Bima ya Afya.

Mkurugenzi wa Mfumo Habari, Ali Othuman anasema kuwa Kurugenzi ya Mifumo Habari  ina lengo la kuhakikisha kuwa mfuko unatumia teknolojia katika mfumo mbalimbali ili kuongeza ubora naufanisi wa kazi.

Kwa mujibu wa Othuman, NHIF imeweka Mfumo wa Usajili Advanced Membership Management Information System (AMMIS), ili kuwezesha usajili wa wanachama, waajiri, utaratibu wa michango ya wanachama,utengenezaji na utaratibu wa vitambulisho vya wanachama.

“Kupitia mfumo huu, Mfuko umerahisisha kazi za utoaji vitambulisho kwani sasa kazi ya utayarishaji wa  vitambulisho kwa kiasi kikubwa zinafanywa kwenye ofisi zetu za mikoa,” alieleza Othuman.

Anaongeza kuwa mfumo mwingine ni mfumo wa utambuzi wa wanachama katika vituo vya huduma (Online Verification) ambao hutumika kuwatambua wanachama kabla ya kupata huduma kwa kuoanisha michango ya mwezi na uhalali wa mwanachama ambapo Mfuko unaweza kuwatambua wanachama wake halali wanaostahili kupata huduma katika dirisha la kutolea huduma.

Anasema kuwa mfumo mwengine ni wa ulipaji wa madai ya watoa huduma za Matibabu ujulikanao kama Claims Management Information Systems (CMIS) ambao unawezesha mfuko kutengeneza malipo ya watoa huduma kwa usahihi, umakini mkubwa na kwa uharaka.

Anaongeza kuwa mwingine ni Financial Management Information Systems  (FMIS) ambapo unasaidia usimamizi wa fedha kwa mfuko na kuonesha ufanisi mkubwa katika kutunza kumbukumbu za makusanyo na malipo, kuzuia udanganyifu katika kukusanya mapato au kulipa pamoja na kuweka kumbukumbu ya mali za shirika (assets). Faida kubwa ya mfumo huu ni kuwa umefunganishwa na mifumo mingine ya Mfuko.

“Kipo pia  kituo cha kuhifadhi na kuchakata kumbukumbu, ambapo mfuko  umeweza Kuweka na kuhifadhi  kumbukumbu kwa njia ya eletroniki pamoja na nyaraka za mfuko zipo katika mifumo zimehifadhiwa katika utunzaji mbadala wa kilaini
(soft copy).

Mfumo mwingine uliopo ni  wa utoaji wa vibali kwa ajili ya huduma maalum (Service authorization) ulioundwa kwa ajili ya kutoa vibali vya huduma mbalimbali kwa wanachama kama dawa za saratani, dawa kwa wagonjwa waliopandikizwa figo bandia  na nyingine, vipimo kama MRI , miwani na vifaa saidizi.

Anasema mfumo huu umesaidia wanachama kutotembea umbali mrefu kutoka kwenye vituo walipo mpaka kwenye ofisi za mfuko kwa ajili ya huduma pia umesaidia kupunguza msongamano wa kusubiri huduma za vibali katika ofisi za mfuko.

Anasema ili kutambua ukiukwaji wa shughuli za mfuko, Menejimenti imewekeza katika mfumo wa kuwa na kituo cha kisasa cha kutayarisha takwimu na taarifa kwa kasi ili kazi zote ziende haraka na kwa ufanisi kwa saa 24.

Hata hivyo, Othuman anasema kuna changamoto kubwa katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kiteknohama katika vituo hivyo basi mfuko umeamua kwa dhati kuweka mkopo nafuu wa kukopesha vifaa vya ICT kwa watoa huduma na kusaidia pale itabidi kuweka vifaa vya ulazima kwa vituo vya Serikali.

Anasema matarajio ya baadaye kuanza kutumika kwa vitambulisho vya utaifa katika utambuzi wa wanachama wa mfuko ambapo itasaidia katika utambuzi wa madai ya kughushi na kuokoa gharama za kuendelea kutengeneza vitambulisho mara kwa mara.

Pia kuwekeza katika mifumo ya hospitali ambapo mfuko kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itawekeza katika mifumo ya ICT hospitalini ili kupunguza gharama za upotevu wa dawa, makaratasi na kuhakikikisha mfuko unalipa malipo
halali.

Anasema kuweka kituo cha mawasiliano ( H u d u m a kwa Wateja) ambapo mfumo unategemea karibuni kuanzisha kituo cha mawasiliano ambayo wanufaika watakuwa muda wote wana uwezo wa kupiga simu na kueleza changamoto zao.

Wasemavyo watoa huduma Akizungumzia Mfumo huu Mkrugenzi wa Fedha katika Hospitali ya KCMC Kilimanjaro, Bi. Hilda Mungure alisema kuwa mfumo huu umerahisha utambuzi wa wanachama wa Mfuko pamoja na kuondoa mianya yote ya udanganyifu.

“Kwa mfumo huu hakuna kuchomekea…huduma zinatolewa kwa walengwa kutokana na Mfumo wenyewe kuwatambua hivyo una faida kubwa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika kudhibiti malipo hewa,” alisema Mungure.

Kwa upande wake Dk.Emmanuel Athanas wa Kliniki ya Watoto iliyopo Sinza Dar es Salaam,anasema k uwa Mfumo wowote huwa una changamoto za hapa na pale katika kuutumia hivyo akasisitiza mafunzo kwa watumiaji.

Anasema kuwa Mfuko ukiachana na changamoto ndogo zilizopo, Mfumo ni wa uhakika zaidi kwa pande zote mbili ya mtoa huduma na Mfuko
wenyewe kwa kuwa huwezi kuingiza kitu chochote kilicho nje na taarifa za mwanachama.