Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanzisha mpango mpya wa huduma za matibabu kwa watoto chini ya umri wa miaka 18 ambao unajulikana kwa jina la “Toto Afya Kadi” kwa lengo la kuwawezesha watoto kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote.

NHIF-Toto Afya Kadi ni nini?

Ni kadi ya Bima ya Afya ya NHIF inayotolewa kwa watoto wa chini ya miaka 18 anaosajiliwa na NHIF ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Madhumuni ya kuanzisha Toto Afya Kadi.
  • Ili kutoa fursa kwa wazazi/walezi ambao ni wanachama wa Mfuko kusajili watoto ambao hawakuweza kusajiliwa kwa sababu nafasi za wategemezi za mwanachama zimejaa, kwa mfano mwanachama ana watoto 6 lakini nafasi za wategemezi zilizopo ni 4 tu.
  • Kutoa nafasi kwa watoto ambao hawana uhusiano wa damu na mwanachama mchangiaji kujisajili kupata huduma kwa kuingizwa na mzazi au mlezi mfano, mtoto wa shangazi n.k
  • Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata Bima ya afya kupitia wafadhili na wahisani mbalimbali.
Walengwa ni nani?
  • Watoto wote wa shule za awali, msingi na sekondari.
  • Watoto wa kutoka vituo vya kulea watoto yatima na wasiojiweza,
  • Watoto waishio na wazazi/walezi bila kujali uhusiano walionao na kama wanasoma shule, au hawasomi.
Watanufaika na nini?
  • Watapata matibabu yote katika vituo zaidi ya 6000 nchi nzima, Watapata mafao yote NHIF ya matibabu kuanzia kumuona daktari, vipimo, dawa, kulazwa, upasuaji mdogo na wa kitaalamu, mazoezi ya viungo, vifaa saidizi, matibabu ya macho na kinywa.
Jinsi ya kujisali.
  • Fomu ya usajili itajazwa na kubandikwa picha ya mtoto ya ukubwa wa pasipoti.
  • Kuchangia ni mara moja kwa mwaka kiasi cha 50,400.00 kwa mtoto mmoja.
  • Kujisajili tembelea Ofisi ya NHIF iliyo karibu au wasiliana -Huduma kwa wateja bila malipo kwa namba  - 0800 110063, au barua pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.