Nini faida za Mfuko wa Afya ya Jamii ?
Mwanachama atanufaika na huduma zote za afya ya msingi za kinga na tiba zitolewazo katika zahanati, kituo cha afya na hospitali ya Wilaya kama vile:

  •     Huduma ya wagonjwa wa kutwa na kulazwa.
  •     Vipimo vya maabara.
  •     Huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri husika.
  •     Wanachama wanapata huduma bora ya afya mwaka mzima.
  •     Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata malipo ya tele kwa tele toka Serikali ambayo yanatumika kuboresha huduma za afya.

Je naweza kupata huduma ya tiba moja kwamoja katika hospitali ya wilaya?
Ndiyo, endapo unaishi karibu na hospitali. Unaweza kupata huduma za tiba za msingi, iwapo kama tatizo ni kubwa unatakiwa kufuata taratibu za wagonjwa wanaohamishwa kutoka zahanati/kituo cha afya kwenda hospitali.

Matumizi ya fedha za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa;

  •     Dawa (suala la dawa ni la muhimu sana);
  •     Vifaa tiba muhimu;
  •     Uboreshaji wa miundo mbinu ya afya;
  •     Ajira ya muda panapokuwa na upungufu hasa wa wataalamu wa kutoa huduma za afya

Je watoto wangu wanaweza kupata huduma kupitia CHF ?
Ndiyo, kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano watapata huduma bure kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Je Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) unaweza kuhudumia watoto wangu wote?
Ndiyo, unaweza kuhudumia watoto katika familia,hii ikiwa ni watoto walioko katika kaya iliyojiandikisha ambao umri wao ni chini ya miaka 18.

    Ndiyo, wanaweza. Watasajiliwa kama wanachama wa CHF, na watajiunga katika makundi kulingana na mwongozo.
    Waalimu wakuu wawasiliane na waganga wakuu wa kituo ili kupata mwongozo zaidi.