NHIF Dodoma yapongezwa kwa kuongeza Ufanisi

Imewekwa: 13 October, 2025
NHIF Dodoma yapongezwa kwa kuongeza Ufanisi

13 Oktoba, 2025

Hayo yamejiri wakati Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. Irene C. lsaka alipokutana na watumishi wa NHIF  Ofisi ya Mkoa wa Dodoma  kwa ajili ya kikao kazi.

Pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi Mkuu alipokea taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko kwa Mkoa wa Dodoma kwa Kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025_26 yaani Julai hadi Septemba 2025. Mkurugenzi Mkuu alionesha kuridhishwa na kasi ya uchakataji madai kwa watoa huduma, ambapo kwa sasa madai yanalipwa kwa wastani wa siku 25 ikilinganishwa na hapo awali ambapo malipo yalilipwa kwa wastani wa siku 77.

Dkt. Isaka aridhishwa na utendaji wa robo ya kwanza hasa kwenye eneo la ukusanyaji michango pamoja na mikakati iliyowekwa kuwafikia Wakulima, wafanyabiashara na wanafunzi.

Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuwahimiza watumishi kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa, hususani tunapoelekea katika utelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote.

Watumishi walipata wasaa wa kuwasilisha changamoto na maoni mbalimbali ili kuboresha utendaji wa Taasisi na Mkurugenzi  Mkuu alitoa ufafanuzi na kuahidi kufanyia kazi changamoto zilizowasilishwa.

Mwisho,watumishi walimuahidi Mkurugenzi Mkuu kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha lengo la Taasisi na matarajio ya nchi kwa ujumla.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa