Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeibuka mshindi wa tuzo ya uwazi na uwajibikaji katika Hafla ya Tuzo za Ubunifu katika Utumishi wa Umma (Public Service Ssrvice Innovation Awards) iliyofanyika tarehe 16 Desemba 2025, jijini Dar es Salaam.
Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Lembris Laanyuni aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Dkt. Irene C. Isaka akitoa neno la shukrani mbele ya Mgeni Rasmi alisema, NHIF imepokea tuzo hiyo kwa unyenyekevu mkubwa kwakuwa tuzo hiyo imetambua juhudi za Mfuko katika kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na uwajibikaji hasa katika kipindi hiki tunapoendelea na utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
Tuzo hii imekuja sambamba na tuzo nyingine ya ushindi wa kwanza kwa Mfuko katika Ufungaji Bora wa Mahesabu toka NBAA. Tuzo hizi mbili zinaonesha namna Mfuko ulivyojipanga kuhudumia wanachama na wadau kwa viwango vya juu, alisema Bw. Laanyuni.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji Ndugu Khamis Suleiman Mwalim, alisema kuwa tuzo hiyo iwe chachu kwa watumishi wa Mfuko katika kuongeza ubunifu na utendaji wenye tija kwa maendeleo ya Taifa. Tuzo hizi za kwanza za Ubunifu katika Utumishi wa Umma ni hatua muhimu kuelekea kuimarisha huduma za NHIF na kufanikisha dhamira ya Bima ya Afya kwa Wote.
Tuzo hii mliyopata mwaka huu ikawe ni mwanzo wa kupokea tuzo nyingine miaka ijayo, na hili litawezekana tu pale mtakapoendelea kutekeleza majukumu yenu kwa bidii na maarifa mkizingatia sekta nyeti mnayohudumu, alisema Bw. Mwalim.
Awali waandaaji wa tuzo hizo "Public Service Innivation Awards" waliekezea vigezo vilivyotumika kupata mshindi kwa kika tuzo. Kwa upande wa NHIF, tuzo ga Uwajibikaji na uwazi imetolewa baada ya Mfuko kuonesha umahiri katika kuzingatia utawala bora, wakati wa utekelezaji wa majukumu yake. NHIF imekuwa mstari wa mbele kushirikisha wadau na pia Mfuko umekuwa unafanya majukumu yake kwa uwazi na kutenda haki kwa wadau wote, alisema mwandaaji wa tuzo hizo.
Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa