Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo umezindua huduma ya Mkoba ya Madaktari Bingwa wa magonjwa mbalimbali wilayani Mafia. Huduma hiyo itatolewa kwa wiki nzima na Madaktari Bingwa kutoka Muhimbili katika Hospitali ya Wilaya ya Mafia.