Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Agrey Mwanri leo amegawa vitambulisho 171 vya NHIF kwa wakulima waliojiunga na Ushirika Afya na Vitambulisho 43 vya Toto Afya Kadi kwa watoto katika hafla fupi iliofanyika Mkoani Tabora. Ameipongeza NHIF kwa kuwafikia wakulima na watoto kwa bima ya afya.