Wananchi wanaendelea kujitokeza kwa wingi katika banda ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kujiunga na Mfuko huo katika Maonesho ya Saba Saba yanayoendelea. Huduma hizo ziko ndani ya banda la Benjamin Mkapa katika viwanja vya maonesho ya biashara barabara ya Kilwa.