Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imesaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa Tumaini la Mama kwa awamu ya tatu itakayoishia 2020 na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW). Mradi huo wenye thamani ya EURO Mil 13 sawa na TZS. Bil 32.7 una kusudi la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kuwapatia wajawazito bima ya afya