NHIF TOTO AFYA KADI

Katika kutanua wigo wa uanachama, NHIF sasa inasajili watoto katika huduma zake ijulikanayo kama NHIF TOTO AFYA KADI.

NHIF-Toto Afya Kadi ni nini?

Ni kadi ya Bima ya Afya ya NHIF inayotolewa kwa watoto wa chini ya miaka 18 wanaosajiliwa na NHIF ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Madhumuni ya kuanzisha Toto Afya Kadi;

 • Ili kutoa fursa kwa wazazi/walezi ambao ni wanachama wa Mfuko kusajili watoto ambao hawakuweza kusajiliwa kwa sababu nafasi za wategemezi za mwanachama zimejaa, kwa mfano mwanachama ana watoto 6 lakini nafasi za wategemezi zilizopo ni 4 tu.
 • Kutoa nafasi kwa watoto ambao hawanauhusiano wa damu na mwanachama mchangiaji kujisajili kupata huduma kwa kuingizwa na mzazi au mlezi mfano, mtoto wa shangazi n.k
 • Watoto ambao wazazi wao hawana uwezo au wasio na wazazi/ walezi lakini wafadhili au wahisani wangependa kuwalipia matibabu ili nao wapate Bima ya Afya.

Walengwa ni nani?

 • Watoto wote wenye umri chini ya Miaka 18

Watanufaika na nini?

 • Matibabu katika vituo zaidi ya 6000 vilivyo sajiliwa na Mfuko nchi nzima.
 • Watapata huduma zote isipokua huduma za vibali maalum kwa mwaka wa kwanza

Jinsi ya kujisajili;

 • Fomu ya usajili itajazwa na kubandikwa picha ya mtoto ya pasipoti.
 • Ambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa.
 • Nakala ya kitambulisho cha mdhamini wa Mtoto.
 • Kuchangia ni mara moja kwa mwaka kiasi cha 50,400/= kwa mtoto mmoja.
 • Mwanachama ataanza kupata huduma baada ya siku 21 za kujiunga.
 • Kujisajili tembelea Ofisi ya NHIF iliyokaribu nawe katika mikoa yote nchini.
 • Kwa taarifa zaidi wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja simu bila malipo -0800110063
 • -info@nhif.or.tz