Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara
- Mtu anawezaje kupata fao la wastaafu?
-
JIBU: Fao la wastaafu linawahusu wanachama wastaafu wa NHIF waliojiunga kupitia ajira zao. Ili kupata fao la wastaafu mchangiaji anapaswa awe amefikisha umri wa miaka 55 ua 60 na awe amechangia Mfuko kwa muda wa miezi 120 (miaka kumi). Endapo amechangia pungufu ya hapo atatakiwa kulipa kiasi cha fedha kulingana na hesabu inyohusisha miezi iliyopungua. Ili kujisajili kama mstaafu atatakiwa kurudisha kadi yake pamoja na za wategemezi wake wote. Atajaza fomu ya wastaafu na kuambatanisha barua yake ya ustaafu. Atabandika picha yake pamoja na ya mwenza na kisha wataingizwa katika mfumo wa fao la wastaafu.
Kwa kila kadi ya mtegemezi iliyopotea atatakiwa kulipa gharama ya Shilingi 20,000.
- Mwanachama anapopoteza kitambulisho nini cha kufanya?
-
JIBU: Endapo kadi imepotea, mchangiaji atatakiwa apate ripoti ya kupotea kwa kadi kutoka polisi pamoja na barua ya kuomba kadi nyingine kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kisha atajaza formu nyingine atakayobandika picha yake.
Gharama ya kupata kadi nyingine ni Shilingi 20,000 kwa mara ya kwanza na kama ikipotea zaidi ya mara moja atatakiwa kulipa kiasi cha Shilingi 50,000
- Ni viambatanisho gani vinahitajika wakato wa kusajili wategemezi?
-
Ili kupata kitambulisho cha matibabu, hakikisha umejaza fomu yako kikamilifu ikiambatanishwa na picha moja kwa kila mtegemezi anayetambulika kulingana na taratibu zilizopo. Fomu yako iwe na nakala ya viambatisho vifuatavyo cheti cha ndoa kama umeandikisha mume au mke,vyeti ya kuzaliwa kama umeandikisha watoto, cheti chako / cha mwenza wako cha kuzaliwa kama umeandikisha wazazi. Cheti cha kuasili kama umeandikisha uliowaasili.Wasilisha fomu yako kwenye ofisi ya NHIF Iliyokaribu na we.
- Nifanye nini nikitaka kujisajili?
-
JIBU: Utatakiwa kujaza fomu na kuweka viambatanisho kulingana na aina ya uanachama unayotaka kujisajili. Fomu zinapatikana kwenye ofisi za NHIF ua kwenye tovuti hii. Unashauriwa kuwasiliana na kituo cha huduma kwa wateja simu namba 0800 110063 ili kupata maelekezo zaidi.
- Ni Hospitali zipi ninaweza kutibiwa nikiwa na kadi ya NHIF?
-
JIBU: Mwanachama wa NHIF tapata matibabu katika vituo zaidi ya 7000 vilivyosajiliwa na NHIF Tanzania bara na Zanzibar. Kuanzia zahanati hadi Hospitali za rufaa za mikoa, kanda na Taifa zikiwa ni za serikali, binafsi, madhehebu ya dini na maduka ya dawa. Kupata orodha ya vituo fuata link kwenye tovotu hii.
- Mafao gani Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatoa kwa wanachama wake?
-
JIBU: Mwanachama wa NHIF atanufaika na;
1. Ada ya kujiandikisha na kumwona daktari,
2. Huduma ya dawa
3. Huduma za vipimo
4. Huduma za wagonjwa wa n je na kulazwa.
5. Huduma za upasuaji mdogo, mkubwa na wa kitaalamu.
6. Huduma ya tiba ya kinywa na meno.
7. Huduma ya tiba ya macho.
8. Huduma za miwani ya kusomea kwa mwanachama mchangiaji
9. Huduma za mazoezi ya kimatibabu ya viungo.
10. Matibabu kwa wanachama wastaafu na wenza wao bila kuendelea kuchangia (kwa waliokuwa wanachama kupitia ajira zao).
11. Vifaa tiba saidizi kama vile fimbo nyeupe, magongo ya kutembelea, vifaa vya usikivu vifaa shinikizi.
Habari Mpya
Matukio Mpya
-
17 Oct
-
19 Jul
-
02 May