Nawezaje kupata fao la Mstaafu?

  • Fao la wastaafu linawahusu wanachama wastaafu wa NHIF waliojiunga kupitia ajira zao.Ili kupata fao la wastaafu mchangiaji anapaswa awe amefikisha umri wa miaka 55 ua 60 na awe amechangia Mfuko kwa muda wa miezi 120 (miaka kumi). Endapo amechangia pungufu ya hapo atatakiwa kulipa kiasi cha fedha kulingana na hesabu inyohusisha miezi iliyopungua. Ili kujisajili kama mstaafu atatakiwa kurudisha kadi yake pamoja na za wategemezi wake wote. Atajaza fomu ya wastaafu na kuambatanisha barua yake ya ustaafu. Atabandika picha yake pamoja na ya mwenza na kisha wataingizwa katika mfumo wa fao la wastaafu.
  • Kwa kila kadi ya mtegemezi iliyopotea atatakiwa kulipa gharama ya Shilingi 20,000.