Nifanye nini ili nipate kadi nyingine baada ya kupoteza niliyo nayo?

  • Endapo kadi imepotea, mchangiaji atatakiwa apate ripoti ya kupotea kwa kadi kutoka polisi pamoja na barua ya kuomba kadi nyingine kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kisha atajaza formu nyingine atakayobandika picha yake. Gharama ya kupata kadi nyingine ni Shilingi 20,000 kwa mara ya kwanza na kama ikipotea zaidi ya mara moja atatakiwa kulipa kiasi cha Shilingi 50,000