JUKWAA LA WAHARIRI LAPONGEZA UTENDAJI WA NHIF

JUKWAA LA WAHARIRI LAPONGEZA UTENDAJI WA NHIF Dec 06, 2024

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika kuimarisha uhimilivu wa Mfuko na uboreshaji wa huduma kupitia mifumo ya TEHAMA.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa TEF Bw. Deodatus Balile wakati wa kikao kazi kati ya NHIF na Wahariri wa vyombo vya habari nchini.

"Niwapongeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya, tumeona hapa uhimilivu umetoka miezi sita hadi mwaka mmoja, kwa mipango mliyoieleza hapa hatuna mashaka kuwa tunakokwenda ni kuzuri zaidi, tumefurahishwa pia na maboresho ya mifumo ambayo yanakwenda kuondoa changamoto nyingi zilizokuwepo," alisema Bw. Balile.

Akiwasilisha mada ya hali ya Mfuko, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka, alieleza kuwa Mfuko uneweka nguvu katika uboreshaji wa Mifumo ili kuwa tayari kuwahudumia wananchi wengi zaidi kupitia Bima ya afya kwa wote.

"Tumeweka nguvu kubwa katika mifumo ili ihudumie wananchi kwa wakati kwa wao kujihudumia na iweze kuchakata madai ili kulipa madai kwa wakati," alisema Dkt. Isaka.

Akizungumzia utekelezaji wa Bima ya Afya kwa wote, alisema Mfuko umeanza kutekeleza kupitia kundi la wanafunzi na unaendelea na utoaji wanelimu kwa makundi mbalimbali ili wananchi wawe na uelewa wa kutosha na wajiunge ili wawe na uhakika wa matibabu bila kikwazo cha fedha.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge sasa