MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFURAHIA HUDUMA ZA NHIF

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFURAHIA HUDUMA ZA NHIF Nov 30, 2017

Katika maonesho ya Wiki ya Vijana na Uzimaji wa Mwenge Makamu wa Rais wa pili Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa Maonesho hayo aliupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kutoa Elimu bure kwa wananchi wa Zanzibar kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza kama Shinikizo la Damu (BP), Sukari na uwiano wa Uzito na Urefu, lakini pia kwa upimaji wa magonjwa hayo bure.

Alisisitiza NHIF isiishie kwenye Maonesho hayo lakini iwe ikitoa huduma hiyo mara kwa mara pindi Mfuko upatapo fursa ya kufanya hivyo, vilevile Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Mfuko na Fao jipya la TOTO AFYA KADI kwani gharama yake ni nafuu, tofauti na gharama za matibabu ya afya mahospitalini aliuasa Mfuko uhamasishe fao hilo ili watu waweze kujiunga kwa wingi, kwani watoto ni Taifa la kesho, ili waweze kufikia malengo yao wanahitaji uhakika wa Afya zao.