# Tumefanikiwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika shughuli za Mfuko ili kuimarisha utendaji na tija.
# Mwananchi anaweza kujisajili ili kujiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya kwa kutumia mfumo wa TEHAMA.
# Mwanachama anaweza kupata huduma za afya kupitia namba yake ya NIDA si lazima awe na nakala ngumu ya kitambulisho cha NHIF.
NHIF ina mfumo wa kutambua utendaji wa watumishi wake kutumia TEHAMA
#Mfumo wa madai ya watoa huduma wetu unachakata madai yote na una uwezo wa kufanya uchambuzi wa taarifa zilizowasilishwa za madai na KUTHIBITI udanganyifu.
#Malipo ya watoa huduma yanafanyika kwa wakati kwa sababu ya uwepo wa mifumo ya TEHAMA.
# KIPINDI CHA AWAMU YA 6 Madai ya watoa huduma za afya yanafanyika ndani ya siku 45 - 60 ikilinganishwa na siku 120 HAPO AWALI.
#Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita tumesajili wanachama milioni 2.2
#Ukusanyaji wa michango umefikia trilioni 2.3 kutokana na maboresho yaliyofanyika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.
#Ulipaji malipo ya watoa huduma unafanyika kwa wakati.
#Shilingi trilioni 2.29 zimelipwa kwa watoa huduma waliohudumia wanachama wa NHIF. KATI YA HIZO 37% VITUO VYA SERIKALI: 35% VlTUO BINAFSI NA 28% VITUO VYA DINI
# Bilioni 91 zimelipwa kwa watoa huduma waliohudumia WANACHAMA Wastaafu.
#Bilioni 22 zimeokolewa kutokana na UDHIBITI WA udanganyifu wa baadhi ya wanachama, VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA.
# Watumishi 36 wa vituo vya kutolea huduma WALIOHUSIKA NA UDANGANYIFU WAMEWASILISHWA KWA MAMLAKA HUSIKA
# HADI KUFIKA DISEMBA,2024 *Mfuko una ziada ya bilioni 95 ikilinganishwa na nakisi ya bilioni 120 KABLA YA SERIKALI YA AWAMU YA 6.
# MFUKO UMEKOPESHA vituo vya kutolea huduma kwa kuwakopesha vifaa TIBA, DAWA NA miundombinu, hii ni kwa vituo vya Serikali na binafsi.
# Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi, kiasi cha mikopo kilichotolewa ni bilioni 19.
#Mwelekeo wa NHIF ni kutumia TEHAMA kuendelea kuimarisha huduma zake kwa wananchi ili kurahisisha utoaji wa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi.
#NHIF inakwenda kusajili makundi kama wakulima, wajasiriamali na mengine.
# TunawaHAMASISHA WANANCHi ya kujiunga na Bima ya Afya, msisubiri hadi mnapokuwa wagonjwa ndipo mshughulikie kupata Bima ya Afya. Nasisitiza kuondoa dhana ya kwamba Bima ya Afya ni uchuro.
#TUTAWASILIANA NA UTPC kuwasajili waandishi wa habari wote ambao ni wakujitegemea ili waweze kuwa wanufaika ili kupata huduma ya Bima ya Afya.
# MFUKO UNATEKELEZA BIMA YA AFYA KWA WOTE KWA KUANZA USAJILI WA VIKUNDI HASA WAKULIMA, WAFUGANI WACHIMBAJI WADOGO, WAVUVI, WAJASIRI AMALI. TAYARI MFUKO UNAENDELEA KUSAJILI WANAFUNZI.
KWASASA MFUKO UNASHIRIKIANA NA OFISI YA RAIS TAMISEMI, NBS NA TASAF, KWA AJILI YA UTAMBUZI WA KAYA ZISIZO NA UWEZO KWA AJILI YA KUHAKIKISHA WANANCHI WOTE WANAPATA BIMA YA AFYA.
#KATIKA AWAMU YA 6 IDADI YA VITUO vya kutolea huduma IMEONGEZEKA kufikia 10,004.