NHIF YAKUTANA NA WAHARIRI KATIKA KIKAOKAZI KUADHIMISHA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KWAKE

NHIF YAKUTANA NA WAHARIRI KATIKA KIKAOKAZI KUADHIMISHA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KWAKE Aug 29, 2021

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa akifungua Kikao Kazi cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF na Wahariri wa Vyombo vya Habari kinachofanyika kwenye ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma leo Jumamosi Agosti 28,2021 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa (NHIF) nchini Tanzania.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernald Konga akimkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa ili kufungua kikao kazi hicho ikiwa ni maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa (NHIF) nchini Tanzania.

Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Angella Mziray akiwasilisha ratiba ya kikao kazi hicho kinachofanyika kwenye ukumbi wa PSSSF jijini Dododma leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile wakiwa katika mkutano huo.

Wahariri Joyce Njalabi kulia kutoka Uhuru Media na Grace Kingalame kutoka TBC wakifuatilia mada katika kikaokazi hicho.

Mmoja wa Wahariri Tausi Mbowe akifuatilia mada katika kikaokazi hicho.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa akikata keki kuashiria maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa (NHF) nchini Tanzania huku Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernald Konga katikati na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile wakipiga makofi.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernald Konga na na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile wakibadilishana keki kuashiria maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa (NHF) nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa akigawa keki kwa Mmoja wa wahariri Bi. Tausi Mbowe ambapo keki hizo zimegawiwa kwa wahariri mbalimbali waazilishi walioandika habari na makala mbalimbali wakati (NHIF) ikianzishwa nchini Tanzania

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernald Konga na na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile wakiwa katika picha ya pamoja na wahariri mbalimbali waazilishi walioandika habari na makala mbalimbali wakati (NHIF) ikianzishwa nchini Tanzania.

Baadhi ya wakuuu wa Vitengo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF wakisikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa hayupo pichani wakati akifungua kikao kazi hicho

Picha zikionesha Baadhi ya baadhi ya wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi wa habari waandamizi wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa wakati akifungua Kikaokazi hicho leo.