NHIF YAZINDUA MPANGO WA DUNDULIZA KWA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA KUPITIA BENKI YA NMB

NHIF YAZINDUA MPANGO WA DUNDULIZA KWA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA KUPITIA BENKI YA NMB Nov 02, 2020

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Benki ya NMB wamezindua mpango unaojulikana kwa jina la DUNDULIZA unaomwezesha mwananchi kudunduliza fedha kidogo kidogo za mchango wa bima ya afya na hatimaye kufanikisha kuchangia kiwango kinachotakiwa na kujiunga na huduma za bima ya afya kupitia NHIF.

Uzinduzi huu umefanyika leo tarehe 05 Oct, 2020 Dar es Salaam ambapo pia uzinduzi huo umeambatana na kusaini makubaliano (MOU) kati ya NHIF na Benki ya NMB ya namna wateja watakavyoweza kuchangia ama kujiwekea fedha kwa ajili ya kukamilisha mchango wa huduma anazohitaji.

Mpango huu umelenga kuwawezesha wananchi wanaojiunga na NHIF kupitia mpango wa Vifurushi kuweka fedha kidogo kidogo kupitia Benki ya NMB kwa muda atakaochagua na atakapokamilisha kiwango husika atapatiwa kadi ya matibabu na kuanza kunufaika na huduma za matibabu kupitia NHIF.


Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna katikati na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto Bw. Bernald Konga wakionesha kadi ya Dunduliza baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa huduma ya Dunduliza itakayomfanya mteja kujiwekea fedha na baada ya kutimiza malengo atapatiwa kadi ya bima ya afya kulia ni anayeshuhudia ni Filbert Mpozni Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernald Konga akibadilishana mkataba na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano katika uotaji wa huduma ya bima ya afya kupitia huduma ya Dunduliza leo katika ofisi za NHIF mkoa wa Kinondoni jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernald Konga akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo leo katikati ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna na kulia ni Filbert Mponzi Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB.


Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba huo kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernald Konga na kulia ni Filbert Mponzi Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna katikati na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto Bw. Bernald Konga wakisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa huduma ya Dunduliza itakayomfanya mteja kujiwekea fedha na baada ya kutimiza malengo atapatiwa kadi ya bima ya afya kulia anayeshuhudia ni Filbert Mponzi Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna katikati na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto Bw. Bernald Konga wakionesha mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa huduma ya Dunduliza itakayomfanya mteja kujiwekea fedha na baada ya kutimiza malengo atapatiwa kadi ya bima ya afya kulia anayeshuhudia ni Filbert Mponzi Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB na kushoto ni Christopher Mapunda Mkurugenzi wa Wanachama NHIF.