NHIF Yazindua Mpango wa Toto Afya Kadi

NHIF Yazindua Mpango wa Toto Afya Kadi Nov 30, 2017

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa bima ya afya ya Mtoto 'Toto Kadi' leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa kiu yake katika sekta ya afya ni kuona kila mtu ana bima ya afya.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kadi ya Bima ya Afyakwa Mtoto ‘Toto Kadi’ , amesema kuwa taifa kuwa lina maendeleo linatokana na msingi wa afya ambapo msingi huo unatokana na kuwa watoto wanaopata huduma za afya kwa uhakika.

Amesema kuwa gharama za kulipa matibabu katika ukuaji watoto na hali uchumi ni kubwa lakini kuwepo kwa bima hiyo kutanya wazazi kuwa na furaha wakati wote hata ikitokea ugonjwa bima ndio inamaliza matatizo.

Ummy amesema kuwa wakati anaingia madarakani alikutana na Rais Dk. John Pombe Magufuli alichoendanacho ilikuwa ni kuongeza ghrarama lakini Rais alisema hakuna kuongeza ghrama yeyote cha msingi waangalie jinsi ya kusaidia watanzania kuwa na bima.

Aidha Waziri Ummy amewaomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuja na bima ya mama mjamzito itakayotumika wakati ujauzito na badaa ya kujifungua.

Ummy amesema kuwa kampeni hiyo iwe endelevu kwa nchi nzima ili watoto wote kuwa na bima ya afya hapo tutakuwa tunajenga taifa lenye msingi bora wa afya.Waziri huyo ameitaka kuweka utaratibu wa kubandika mabango katika kila kumbi za starehe ili wanavyotumia vinywaji waweze kuangalia watoto kama wana kadi ya afya bima ya afya.