WAAJIRI LIPENI MICHANGO YA BIMA YA AFYA WATUMISHI WAPATE HAKI ZAO ZA MATIBABU - MHE. SAMIA

WAAJIRI LIPENI MICHANGO YA BIMA YA AFYA WATUMISHI WAPATE HAKI ZAO ZA MATIBABU - MHE. SAMIA May 03, 2023

Na Mwandishi wetu - Morogoro

Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka waajiri nchini kulipa asilimia tatu ya michango ya bima ya afya kwa wakati ili watumishi wapate haki zao za matibabu.

Ameyasema hayo leo akihutubia hadhara ya maelfu ya wafanyakazi, waliojumuika pamoja kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa imefanyika mkoani Morogoro.
"Kuna suala la wale watumishi wanaochangia asilimia tatu lakini mwajiri hapeleki, hili nalo mkaliangalie ili waajiriwa wapate haki zao za matibabu" amesema Mhe. Samia.

Awali akisoma risala ya wafanyakazi, Katibu wa Shirikisho la Wafanyakazi TUCTA Bw. Hery Mkunda alisema mwajiri anapochelewesha michango wa matibabu kwenye bima ya afya, mtumishi ndiye anayepata changamoto ya kukosa huduma za matibabu ili hali ameshakatwa asilimia tatu tayari.


Utaratibu wa bima ya afya kwa watumishi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unamtaka mwajiri kuwasilisha michango ya matubabu ya watumishi ambayo ni asilimia 6 ya mshahara wa mtumishi kila mwezi ambapo aslimia 3 inatoka kwa mtumishi na asilimia 3 kwa mwajiri.