WANAFUNZI WAITIKA KUJIUNGA NA NHIF

WANAFUNZI WAITIKA KUJIUNGA NA NHIF Oct 31, 2024

Wanafunzi kutoka vyuo Vikuu na Shule za Sekondari nchini, wamefurahishwa na Mfumo wa usajili wa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika mwaka huu wa masomo ambapo wamewezeshwa kujisajili wenyewe.

Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na wanafunzi wa vyuo vya DUCE Dar es Salaam, Mzumbe Morogoro, KIHAS Karagwe, Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa na Shule ya Sekondari Ndono mkoani Tabora wakati wa mafunzo ya utumiaji wa Mfumo katika kujisajili na huduma za NHIF.

Mwitikio wa usajili wa kundi la wanafunzi ni mkubwa kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Mfuko hususan katika eneo la usajili wa wanachama ambapo kwa sasa kila mwanafunzi anaweza kujisajili na kuanza kunufaika na huduma za matibabu.

Mfuko unawasajili wanafunzi kuanzia ngazi ya awali hadi Chuo Kikuu kwa kulipa mchango wa shilingi 50,400 na kunufaika na huduma za matibabu katika vituo zaidi ya 9000 vilivyosajiliwa nchi nzima.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa