Huduma za Ziada
UJUE MPANGO WA HUDUMA ZA ZIADA WA NHIF
Ili kuhakikisha huduma bora za matibabu zinapatikana kwa wanachama wake, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanzisha mpango wa huduma za ziada kwa waajiri wanaohitaji huduma hizo.
Kwa kupitia mpango huu mwanachama anapewa fursa ya kuongeza huduma za ziada atakazopenda kulingana na mahitaji yake kwa makubaliano maalumu kati ya mwajiri na NHIF.
WANUFAIKA WA MPANGO HUU
- Waajiri wote waliosajiliwa na NHIF
HUDUMA ZA ZIADA
Mwajiri anayo fursa ya kuchagua huduma za ziada kulingana na mahitaji yake.
Huduma hizo ni pamoja na :-
- Matibabu nje ya nchi
- Uchunguzi wa afya (Medical checkup)
- Malipo ya dawa zenye majina ya biashara (Branded Medicine)
- Gharama za ziada za miwani
- Gharama za kulazwa katika wodi binafsi (Private Ward)
- Huduma za dharura na uokoaji kwa kutumia ndege au gari la wagonjwa (Air and Ground Ambulance)
- Huduma za haraka za matibabu (Fast tracking services)
VIGEZO NA TARATIBU ZA KUJIUNGA NA MPANGO WA HUDUMA ZA ZIADA
Ili mwanachama aweze kunufaika na mpango huu mwajiri anahitajika kuwa na sifa na vigezo vifuatavyo;
- Awe mwajiri aliyesajiliwa na Mfuko,
- Mwajiri atahitajika kuwasilisha barua ya maombi kwa Mkurugenzi Mkuu ikiainisha huduma za ziada anazohitaji.
- Mwajiri atahitajika kulipa malipo ya ziada kwa ajili ya huduma hizo mwanzoni mwa mkataba.