Health Insurance for Private Individual

Mwanachama binafsi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, ni mtu yeyote anayeamua kujiunga na Mfuko huu kwa hiari bila uwepo wa uhusiano baina ya mwajiri na mwajiriwa.

WANUFAIKA WA UTARATIBU HUU

Mwanachama binafsi atapata fursa ya kuwa na wategemezi kama ilivyo kwa mwanachama aliyeajiriwa. Wategemezi wanaokubalika ni wale tu wanaotambulika chini ya utaratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Wategemezi hawa ni pamoja na mwenzi wa mchangiaji, (mke au mume), watoto wa kuzaa au kuasili chini ya miaka 18 au wazazi wa mwanachama mchangiaji na wa mwenza wake

UTARATIBU WA KUJIUNGA

Masuala yafuatayo ya msingi lazima yazingatiwe kabla ya kujisajili;-

 • Mwombaji atajaza fomu ya maombi ya uanachama binafsi
 • Mwombajiatajaza fomu ya uanachama ikiambatanishwa na picha moja za pasipoti za rangi za kwake na kila mtegemezi anayetambulika kisheria;
 • Wakati wa kusajili wategemezi mwombaji awasilishe nyaraka za kisheria zinazoonyesha uhusiano wake na wategemezi aliowaainisha.

Tegemezi

Nyaraka

Mwenza

 • -Cheti cha Ndoa
 • -Nakala ya kitambulisho (Leseni ya udereva, mpiga kura, Kitambulisho cha utaifa au Pasipoti ya kusafiria)

Mtoto

Cheti cha kuzaliwa cha mtoto

Mzazi

 • - Cheti cha kuzaliwa cha mwanachana mchangiaji
 • - nakala ya kitambulisho cha mzazi (Leseni ya udereva, mpiga kura, Kitambulisho cha utaifa au Pasipoti ya kusafiria)

Mzazi wa Mwenza

 • -Cheti cha Ndoa pamoja
 • -Cheti cha kuzaliwa cha mwenza
 • -nakala ya kitambulisho cha mzazI wa mwenza (Leseni ya udereva, mpiga kura, Kitambulisho cha utaifa au Pasipoti ya kusafiria)
 • Vitambulisho vya matibabu vitatolewa kwa kila mtegemezi atakayeainishwa na vitakuwa na ukomo wa matumizi wa mwaka mmoja.
 • Kila mwisho wa muda wa matumizi wa vitambulisho husika, mwanachama atatakiwa kuomba upya uanachama kwa kuchangia kiwango cha mchango kitakachowekwa na Mfuko kwa wakati huo;
 • Mwanachama ataanza kupata huduma siku 21baada ya kukamilisha utaratibu wa kujiunga.
 • Baada ya kadi kuisha muda wake (mwaka moja), mwanachma atatakiwa kuchangia tena ili kuhuisha kadi yake ndani ya siku thelathini (30). Iwapo atachelewa kuhuisha uanachama wake atakosa sifa ya kuendelea na uanachama kwa mwaka wa pili, hivyoatahitajika kujisajili upya

UTARATIBU WA UCHANGIAJI KWA MWANACHAMA BINAFSI

Mwanachama binafsi atachangia kiwango cha TZS 1,501,200 kwa mkupuo mmoja kila mwaka kabla ya kuanza kupata huduma.

UKOMO KWA MWANACHAMA BINAFSI

Mwanachama binafsi na wategemezi wake walioandikishwa, uanachama wao utakoma:-

 • Endapo mwanachama mchangiaji atafariki, hata hivyo wategemezi wa mwanachama wataendelea kupata huduma kwa kipindi kilichosalia ndani ya mwaka husika;
Endapo hatachangia upya kwa awamu inayofuata.