TOTO AFYA KADI

Ni kadi ya Bima ya Afya ya NHIF inayotolewa kwa watoto wa chini ya miaka 18 wanaosajiliwa na NHIF ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Madhumuni ya kuanzisha Toto Afya Kadi:-

  • Kuwapa fursa kwa wazazi/walezi ambao ni wanachama wa Mfuko kusajili watoto ambao hawakuweza kusajiliwa kwa sababu nafasi za wategemezi za mwanachama zimejaa, kwa mfano mwanachama ana watoto 6 lakini nafasi za wategemezi zilizopo ni 4 tu.
  • Kutoa nafasi kwa watoto ambao hawanauhusiano wa damu na mwanachama mchangiaji kujisajili na kupata huduma kwa kulipiwa na mzazi au mlezi mfano, mtoto wa shangazi n.k
  • Kutoa fursa kwa wafadhili au wahisani kuwalipia gharama za usajili watoto walio kwenye mazingira magumu na vituo vya kulelea watoto yatima .

Walengwa ni nani?

  • Watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 18

Watanufaika na nini?

  • Matibabu katika vituo zaidi ya 7000 vilivyo sajiliwa na Mfuko nchi nzima.
  • Watapata huduma zote isipokua huduma za vibali maalum kwa mwaka wa kwanza wa uchangiaji

Jinsi ya kujisajili;

  • Mzazi/ mlezi atajaza Fomu ya usajili na kubandika picha ya mtoto ya pasipoti.
  • Mzazi/ mlezi ataambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mtoto.
  • Mzazi/ mlezi atachangia mara moja kwa mwaka kiasi cha 50,400/= kwa mtoto mmoja.
  • Mwanachama ataanza kupata huduma baada ya siku 21 tangu kukamilisha taratibu za usajili
Huduma za usajili zinapatikana katika ofisi zote za NHIF nchi nzima